Click here for the English version / Bofya hapa kwa toleo la Kiingereza
Mradi wa VNA na programu ya ‘Ulimwengu Wangu wa Kazi’
Utangulizi
Vijana na Ajira (VNA), mradi wa Vijana na Ajira ni moja ya miradi ya VSO, Volunteer Services Oversee (Huduma za Kujitolea, Ng’ambo) kwa ushirikiano na RGZ, (Revolutionary Government of Zanzibar/Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar). Moja ya vipengele vya mradi wa VNA ni programu ya ‘Ulimwengu Wangu wa Kazi’ (UWwK).
Programu ya UWwK hutaka kuimarisha nafasi ya kijamii na kiuchumi ya vijana ndani ya Zanzibar kwa kuendeleza ustadi mbalimbali wanaouhitaji kwa ajili ya ajira, ajira binafsi au ujasiriamali. Kwa kusudio hilo, viunganishi madhubuti zaidi baina ya sekta binafsi na mafunzo ya ufundi ni muhimu. Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi (Amali), NACTE (Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi), Vituo vyote vya Mafunzo ya Ufundi (Amali) na Taasisi za Zanzibar zinahusishwa kama washirika katika programu hii ya UWwK. Wana majukumu makubwa katika kuwawezesha vijana pamoja na ujuzi muhimu kuingia katika soko la ajira.
Programu ya UWwK imezalisha sanduku la zana na masomo mawili muhimu: Mafunzo na Elimu ya Kuzingatia Umahiri na Maendeleo ya Kazi.
Mafunzo na Elimu ya Kuzingatia Umahiri (CBET)
Kutokana na ukweli kwamba MMA na NACTE wamekubali njia za ufundishaji na kujifunza za CBET (Mafunzo na Elimu ya Kuzingatia Umahiri), mwanzo wa sanduku la zana ‘Ulimwengu Wangu wa Kazi’ inarudi kwenye mkutano wa siku moja wa uongozi na siku nne za Mafunzo ya Utangulizi kuhusu CBET. Katika mafunzo haya ya siku nne, makundi manne ya walimu katika ujenzi, viwanda na utalii, Unguja na Pemba walipata Utangulizi kwenye mbinu ya CBET. Kulingana na mafunzo haya, vifaa viliundwa na kugawanywa ili kutekeleza mbinu ya CBET, kipindi cha shughuli zote za programu ya UWwK pamoja na wadau na washiriki. Katika picha inayowakilisha mti, dhana ya CBET inaelezwa. Katika mwongozo (kitabu cha maelekezo) ‘Mafunzo ya Wakufunzi (T-o-T) kuhusu CBET’, masomo yote, mazoezi na vifaa vya mafunzo ya utangulizi juu ya CBET vimejumuishwa.
Maendeleo ya Kazi
Mradi wa VNA una ushirikiano madhubuti na Idara ya Kazi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Maonesho mawili ya kazi yalipangwa pamoja na maonesho ya kiujasiriamali. Programu ya UWwK iliunda vifaa kuhusu Maendeleo ya Kazi: namna ya kuwaongoza vijana katika mafunzo ya ufundi na ajira au ajira binafsi?’ Programu hii ya Mendeleo ya Kazi na zaidi ya mazoezi 130 inawawezesha walimu na wanafunzi kuchagua mazoezi hayo yanoyofaa kwa mahitaji na kiwango cha kundi lao la vijana. Mwongozo (kitabu cha maelekezo) wa Mafunzo ya Wakufunzi (T-o-T) yalianzishwa na wakati huo huo kuungwa mkono na wakufunzi na walimu wa taasisi zote ili waendane na maudhui na uwezeshaji wa mazoezi.
Shukurani!
Mashirika na watu wengi walihusishwa katika shughuli za programu ya Ulimwengu Wangu wa Kazi ya mradi wa VNA. Kulikuwa na mashirika pamoja na wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kulikuwa na viunganisho na kampuni mbalimbali, MMA, NACTE, Vituo vya Mafunzo ya Ufundi (Amali), Taasisi za Ufundi na Mashirika kadhaa yasio ya kiserikali. Ilikuwa ni faida kubadilishana mawazo kuhusu maendeleo na utekelezaji wa sanduku la zana. Wadau na washiriki wote, asanteni sana kwa ushirikiano wenu na uungaji mkono wenu.
Neno la shukurani, liwaendee wakufunzi wasaidizi wa Pemba na Zanzibar ambao waliunga mkono mradi pamoja na ukalimani na uwezeshaji wao wakati wa utoaji mafunzo: Hamed N. Said (MMA), Nafisa Iddi Omar (MMA), Fatma A. Juma (ZIToD) na Saada Ali Hamad (Vitongoji KMAV, Pemba). Mwisho, ni mwalimu wa somo la mawasiliano (Chuo cha mafunzo ya amali Vitongoji Pemba na Mkokotoni Unguja) ndugu Yahya Abdu ambaye ametafsiri sehemu kubwa ya toleo la Kiingereza kwenda Kiswahili, pia amehariri pale palipokua pametafsiriwa tayari.
Shukurani kwa VSO na wenzangu wa mradi wa VNA. Kwanza kabisa, Abraham Mtongole, kiongozi (meneja) wa mradi na washirika ambao walinitambulisha kwa wadau wote na walioniunga mkono pale ilipohitajika. Sophie Oonk, mwenye kujitolea kutoka Randstad Uholanzi ambaye aliendeleza mada ya 5 ‘Gundua biashara yako’ na aliyekuwa mwezeshaji msaidizi wakati wa vipindi vya mafunzo; cha kwanza na cha pili.
Watu wengine wengi sana wamechangia katika hili sanduku la zana: watumishi wa Uholanzi wa kujitolea ambao walifasiri mazoezi ya programu inayohusu Maendeleo ya Kazi mahali pa kwanza na watumishi wa kujitolea kwa mradi wa CASH ambao ulibainisha toleo hilo la Kiingereza. Kwa mpangilio wa kwanza, ilikuwa ni Katie Wolgemuth, VSO Dar es Salaam aliyebuni na wanafunzi wa Grafisch Lyceum Utrecht, Uholanzi walifanya toleo la pili kwa Kiingereza na Kiswahili pia. Mwishoni, ilikuwa ni Kitty den Boogert, rafiki na mwenzangu wa zamani, ambaye alibainisha kwa umakini sasisho la sanduku la zana na kutoa dondoo kwa ajili ya uboreshaji.
Nyote, asanteni sana!
Bila ya shauku yenu, ushiriki ulio na hamasa katika vipindi vya mafunzo na bila ya mawazo yenu ya namna ya kutengeneza programu hii ya UWwK kuwa endelevu, nisingeweza kufanya jitihada zote za kuendeleza hili sanduku la zana.
Wil Bom
Mshauri wa elimu
Februari 2022