Click here for the English version / Bofya hapa kwa toleo la Kiingereza
Mti wa CBET
Mti huu wa CBET ni mfanano kwa mfumo wote wa CBET. Ni picha (ya kuona), bango na hukutaarifu kuhusu vipengele muhimu vya CBET. Miundo yote imefunikwa kwa plastiki (lamination), (muundo wa) A4 na A3, hivyo, inaweza kuwekwa kwenye ukuta katika skuli/shule au kutumika katika vipindi vya mafunzo kwa ajili ya walimu na uongozi.
Mafunzo ya Utangulizi kuhusu CBET
Walimu wa Vituo vya Mafunzo ya Amali na Taasisi za Ufundi walipata Mafunzo ya Utangulizi juu ya ‘nini CBET na namna ya kuwezesha Mafunzo ya Kuzingatia Umahiri? Mafunzo haya ya siku nne kwa makundi 7 ya walimu kutoka Unguja na Pemba. Zingatio lilikuwa ni kuhusu dhana ya CBET (Nini na kwanini?), ujuzi wa kutumia mbinu chochezi (vipi?) na maendeleo ya kazi za vitendo na shughuli za mwongozo wa kazi (ubunifu).
Siku ya 1 Dhana ya CBET
Katika siku hii ya kwanza, washiriki wanajifunza kuhusu CBET na kupata uelewa wa mabadiliko ya dhana kuelekea CBET, ilifafanuliwa katika mada ya 5. Wanabainisha athari za mabadiliko hayo kwa kutathmini taasisi yao wenyewe, ambao hufanya changamoto kubwa zionekane. Wanaweka malengo na shughuli zao kwa kipindi kinachofuata.
- Programu ya siku ya 1 ‘Dhana ya CBET’
- Uwasilishaji ‘Dhana ya CBET’ siku ya 1
- Kitabu cha kumbukumbu siku ya 1 ‘Dhana ya CBET’
- Dhana na mabadiliko ya kanuni za jumla, safu ya MKU (Mafunzo ya Kuzingatia Umahiri) haina kitu
- Dhana na mabadiliko ya kanuni za jumla, safu zote zimejazwa
- Kufanya mapitio ya Taasisi za Mafunzo ya Ufundi ‘kuhama kuelekea MKU’
- Ubao wa maelekezo: Ubao wa mtu mmoja mmoja na kikundi
- Vipaombele katika kuhama kuelekea MKU
- Vipaombele katika kuhama kuelekea MKU (kwa kubandika stika kwenye ukuta)
- Kazi ya vitendo kwa washiriki wa Mafunzo ya Wakufunzi
Siku ya 2 Mbinu chochezi
Washiriki wanatafakari kuhusu mbinu wanazotumia katika madarasa yao. Wanapenda mbinu zipi na kwa nini? Wanajifunza kuhusu mbinu za kuwezesha kwa njia ya CBET na kupata uelewa wa mabadiliko ambayo yanapaswa kufanywa. Wanatayarisha sehemu ya somo kwa njia ya vichocheo na kufanya mazoezi katika kikundi. Kwa pamoja washiriki wote wanatoa mrejesho ‘Nini kilikuwa kizuri?’ na ‘Ni nini kinaweza kuboreshwa?
- Programu ya siku ya 2 ‘CBET na Mbinu chochezi’
- Uwasilishaji ‘CBET na mbinu chochezi’ siku ya 2
- Kitabu cha kumbukumbu siku ya 2 ‘Mbinu chochezi’
- Uwezeshaji na mabadiliko ya mikakati ya kufundishia na kujifunza, safu ya MKU (Mafunzo ya Kuzingatia Umahiri) haina kitu
- Uwezeshaji na mabadilko ya mikakati ya kufundishia na kujifunza, safu zote zimejazwa
- Mbinu za kufundishia na matumizi yake katika MKU
- Pawa pointi Wavunjaji wa barafu, wakazaji wa misuli na kuanza upya
- Mifano ya mbinu chochezi za kujifunza
- Mbinu chochezi za kujifunza
Siku ya 3 Kazi za vitendo
Washiriki wanapata uelewa wa haja ya kufanya mabadiliko kutoka katika nadharia kwenda kwenye kazi za vitendo zaidi, zinazohusiana na mahitaji ya soko la ajira. Wanapata uelewa katika vigezo vya muundo, hufanya mazoezi ya muundo wa mgawo wa kazi za vitendo katika vikundi vidogo na kutafakari juu yao katika kikao.
- Programu ya siku ya 3 ‘CBET na kazi za vitendo’
- Uwasilishaji ‘CBET na kazi za vitendo’ siku ya 3
- Kitabu cha kumbukumbu siku ya 3 ‘Kazi za vitendo’
- Muundo wa shughuli za kujifunza kuhama, safu ya MKU haina kitu
- Muundo wa shughuli za kujifunza kuhama, safu zote zimejazwa
- TEHAMA (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) – Kazi ya vitendo
- Fani ya bomba – Kazi ya vitendo
- Muundo wa kazi ya vitendo
Siku ya 4 Maendeleo ya Kazi
Katika siku hii ya mwisho washiriki wanafahamiana na programu ya ‘Maendeleo ya Kazi’. Katika vikundi vidogo wanachagua zoezi moja kutoka katika mada na wanazifanyia mazoezi kwenye kikundi. Mwishoni kuna tathmini ya mafunzo na kupanga mipango ya utekelezaji na kutoa dondoo namna ya kufanya hivyo.